Umekuwa pia ni mwaka wa mabadiliko kwa Kampuni. Tuliendelea upanuzi wetu Ethiopia, lakini pia tukawa tunatekeleza mkakati wetu mpya wa kuelekea 2030, ili kutimiza ruwaza yetu ya kuwa kampuni ya kiteknolojia inayoongoza Afrika. Bodi inakariri kujitolea kwake kutoa ushauri wa kimkakati na kusaidia wasimamizi wa kampuni wanapotekeleza mkakati wa kampuni na kutimiza lengo letu la Kubadilisha Maisha.
Kwa kweli, upanuzi wa shughuli zetu Ethiopia ni hatua muhimu sana katika mkondo wetu wa ukuaji wa jumla. Tumetiwa moyo na ukakamavu ambao biashara yetu imeuonyesha tangu tulipoufungulia mtandao wetu humo. Muhimu zaidi, tunafurahia kuona biashara yetu Ethiopia ikipiga hatua kuu kama vile ukuaji wa M-PESA, usambazaji wa mtandao wetu, na matumizi makubwa ya data na wateja wetu, miongoni mwa mengine. Tumejitolea kujenga ushirikiano endelevu na kuchangia katika mabadiliko ya kidijitali nchini Ethiopia.
Kwa maelezo zaidi kuhusu shughuli zetu Ethiopia, Bonyeza hapa.
Mazingira ya kisheria na usimamizi yamekuwa yakibadilika kwa haraka, ambapo miongoni mwa mengine kulikuwepo na mabadiliko katika kodi na ada ya kupiga simu kutoka mtandao mmoja hadi mwingine (MTR) nchini Kenya. Lakini tuliendelea kukumbatia mahitaji yanayobadilika ya wadau wetu mbalimbali nchini Kenya na Ethiopia. Inaridhisha kuona mchango wetu katika ustawi wa kijamii na kiuchumi katika mataifa hayo mawili ukiendelea na kuwa wa manufaa.
Kwa maelezo zaidi kuhusu mazingira ambayo tunayudumu, Bonyeza hapa.
Kama wanachama wengine wote wa Bodi, ninajivunia sana lengo la Safaricom la kubadilisha maisha. Inaridhisha kwamba kampuni yetu imeendelea kushiriki moja kwa moja katika kusaidia jamii maeneo tunayohudumu. Hili lilionekana wazi katika mwaka huo kupitia usaidizi ambao tuliutoa kwa watu walioathirika na mafuriko ya hivi majuzi.
Ningependa pia kutambua kazi nzuri ambayo imefanywa na Wakfu wa M-PESA na Wakfu wa Safaricom nchini Kenya katika mwaka tunaouangazia. Nasubiri kuona wanachama wa Bodi wakiendelea kushiriki na kujiunga na wafanyakazi katika shughuli za kusaidia jamii.
Kwa maelezo zaidi kuhusu uwekezaji wetu kwenye jamii, Bonyeza hapa.
Ni furaha yangu kuu kuripoti kwamba Bodi imependekeza mgawo wa faida wa mwisho wa KShs 0.65 kwa kila hisa ya kawaida – ambazo ni jumla ya KShs 24.84 bilioni – ili kuidhinishwa katika Mkutano Mkuu wa Kila Mwaka (AGM). Hii ni juu ya mgawo wa faida wa muda wa KShs 0.55 kwa kila hisa ya kawaida ambao ulitangazwa na kulipwa katika mwaka huo.
Kwa maelezo zaidi kuhusu matokeo yetu ya kifedha, here, na sehemu ya Taarifa za Kifedha za Mwaka katika ripoti hii kuanzia Bonyeza hapa.
Ningependa kusisitiza umuhimu mkubwa ambao tunauweka kwenye uhusiano ambao tunao na wadau mbalimbali. Tunafahamu thamani ya ziada ambayo huletwa na washirika waliojitolea na wenye uwezo.
Hii ndiyo sababu, kama Bodi, katika mwaka huo tuliendelea, kuwashirikisha wadau wetu wote. Tuko imara katika kuhakikisha kwamba mkakati wetu, ruwaza, na lengo kuu vinaonyesha na kutimiza mahitaji na matarajio ya watu binafsi, jamii na wadau ambao huguswa au kuathiriwa na shughuli tunazozifanya kama biashara.
Katika mwaka tunaouangazia, tulidumisha pia mpango wetu wa kuwa na mashauriano mwafaka na watunzi wa sera. Kuhusu hili, bado tumejitolea kushirikiana na serikali, mamlaka zinazosimamia sekta yetu, na wadau wote ili kufanikisha mabadiliko ya manufaa na kuwezesha ukuaji endelevu.
Kwa hivyo, ningependa kutoa shukrani za dhati za Bodi, kwa serikali za Kenya na Ethiopia kwa uungaji mkono wao muhimu. Hakuna shaka kwamba kulainishwa kwa mkakati wetu na ruwaza za mataifa hayo mawili kulikuwa kiungo muhimu katika matokeo yetu ya kuridhisha ya mwaka huu.
Bodi inatambua kujitolea kwa serikali za Kenya na Ethiopia, katika kuunda mazingira mahsusi ya kuchochea ukuaji na uvumbuzi katika sekta ya mawasiliano. Kwa kweli, usaidizi ambao umetolewa na serikali zote mbili umeiwezesha Safaricom kutekeleza mchango wake katika jamii kwa urahisi na kwa njia bora zaidi.
Kwa maelezo zaidi kuhusu mashauriano na uhusiano wetu na wadau, Bonyeza hapa.
Ningependa kutoa shukrani kwa wanachama wenzangu katika Bodi kwa uongozi wao mwema. Ujuzi wao na uongozi wao bora na wa busara vimekuwa muhimu sana katika kuiongoza Safaricom.
Kwa maelezo zaidi kuhusu utawala katika kampuni yetu, Bonyeza hapa.
Katika kipindi kifupi, cha wastani na kirefu, ninatarajia kwamba Safaricom itaendelea kukua na kuimarika zaidi, tunapotekeleza na kutimiza ruwaza yetu ya kimkakati, na kufikisha teknolojia za kisasa kwa watu na jamii tunazozihudumia. Tutaendelea kusaidia uchumi katika mataifa tunayohudumu ambapo huwa tunatekeleza mchango muhimu wa kijamii na kifedha.
Safari ya Safaricom katika mwaka wa kifedha uliopita ni ishara ya uthabiti, uvumbuzi na kujitolea kutimiza lengo letu. Nina uhakika kwamba tunapopanua shughuli zetu Ethiopia na kuendelea kuongoza Kenya, tutaongoza mabadiliko ya manufaa na kuendelea kuunda thamani kwa ajili ya kampuni, wateja na jamii maeneo ambayo tunahudumu.
Ni imani yangu kwamba tutaendelea kuchochea mazingira mazuri ya kibiashara kwa kufanya kazi kwa pamoja na wadau wetu kuhakikisha ukuaji endelevu.
Kwa niaba ya Bodi, kando na shukrani zetu za dhati kwa serikali, wasimamizi wa sekta na bila shaka wadau wote kwa uungaji mkono wao kwetu, ningependa pia kushukuru kundi letu la wasimamizi na watu wote wanaofanya kazi katika Safaricom kwa bidii na kujitolea kwao pamoja na uaminifu wao. Ni bidii yao ambayo imetuwezesha kuandikisha matokeo haya mazuri ambayo tunayaripoti.
Adil Arshed Khawaja (MGH)
Mwenyekiti